Genesis 13:10-13

10 aLutu akatazama akaona lile bonde lote la Yordani kuwa lilikuwa na maji tele, kama bustani ya Bwana, kama nchi ya Misri, kuelekea Soari. (Hii ilikuwa kabla Bwana hajaharibu Sodoma na Gomora.) 11Hivyo Lutu akajichagulia bonde lote la Yordani, akaelekea upande wa mashariki. Watu hao wawili wakatengana: 12 bAbramu akaishi katika nchi ya Kanaani, wakati Lutu aliishi miongoni mwa miji ya lile bonde na kupiga mahema yake karibu na Sodoma. 13 cBasi watu wa Sodoma walikuwa waovu, wakifanya sana dhambi dhidi ya Bwana.

Copyright information for SwhKC